SERIKALI ITAENDELEA KUTHAMINI MICHANGO YA TAASISI BINAFSI

 

 

 

Waziri wa biashara viwanda na masoko mh amina  salum ali amesema  serikali ya mapinduzi ya zanzibar itaendelea kuthamini michango ya taasisi binafsi nchini  hasa katika masuala ya kukuza na  kulea wajasiri amali  wadogo  ambao wengi wao hawana mitaji  ya  kujiendeleza.

Akizungumza baada ya kutembelea   kituo cha  beafoot kinyasini kinachotoa mafunzo  ya ujasili amali kwa  wanawake  wasio  na taaluma amefahamisha kua  elimu inayopatikana hasa katika masuala ya   nishati ya umeme wa sola utawanyanyua  wajasili amali  na kupata mafanikio katika maeneo  wanayoishi.

Meneja wa kituo hicho fatma juma haji na mratibu pendo  jaled  daud  wamesema  mradi huo  una lengo la kuwawezesha wanawake katika masuala tofauti ili wajikwamue na umasikini.

Baadhi ya wajasiri amali wanao patiwa mafunzo hayo wamesema  mafanikio yanayo endelea kuyapata yanatokana  na juhudi za serikali   za kupigania maendeleo hasa  kwa wanawake  ili  waweze kupiga hatua  zaidi.