SERIKALI ITAENDELEA KUWAJENGEA MAZINGIRA MAZURI WAZANZIBAR WANAOISHI NJE

 

Naibu katibu mkuu afisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi zanzibar bi rahma  ali khamis  amesema serikali itaendelea kuwajengea mazingira mazuri wazanzibar wanaoishi nje ili waendelee kuleta misaada yao mbali mbali nchini .Akikabidhi vitabu kwa wizaraya elimu na mafunzo ya amali bi rahma amesema misaada ya wazanzibar hao inanafasi kubwa ya kuchangia maendeleo ya serikali  na kwamba itafanya kila njia ili kuoa misaada hiyo wanaendelea kuleta kwa faida ya wananchi wa zanzibar.Bi rahma ambae  hotuba yake imesomwa na mkurugenzi wa idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ndugu adila hilali ameipongeza jumuiya ya wazanzibari wanaoishi nje kwa kuweka uzalendo mbele kwa taifa lao.Meneja wa jumuiya ya wazanzibari wanaoishi nje kanda ya unguja  bi firdaus rashid rabia amesema jumuiya yake itaendelea kuleta misada huku ikijua mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe.akipokea msada huo wa vitabu mkurugenzi wa elimu msingi na sekondari bi asia iddi  issa amesema wizara ya elimu inathamini msada huo na kufahamisha kwamba umekuja kwa wakati mwafaka.