SERIKALI ITAENDELEZA VITA DHIDI YA UMASKINI ILI KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA MAENDELEO

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imesema itaendeleza vita dhidi ya umaskini ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo katika kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imesema itaendeleza vita dhidi ya umaskini na kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo endelevu ya kuweza kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
Akifungua mafunzo ya uelewa wa mpango wa kunusuru kaya masikini na utekelezaji wake kwa masheha, walimu na maafisa wa afya mkuu wa mkoa wa mjini magharib mh. Ayoub muhammed amewataka watendaji hao kusimamia utekelezaji huo ili kuhakikisha kaya ziliomo kwenye mpango huo zinanufaika kikamilifu.
amesema iwapo watendaji hao watafanya kazi vizuri katika kutoa taarifa sahihi za wahusika hakutotokea malalamiko yoyote kati yao na wananchi .
Naibu katibu mkuu ofisi ya makamu wa pili wa rais ahmada kassim na meneja uhaulishaji fedha kutoka makao makuu ya tasaf dar es salaam omar mlilo,wamesema mtendaji yoyote atakaebainika kufanya vitendo vya udanganyifu atachuliwa hatua za kisheria
Mafunzo ya uelewa wa mpango wa kunusuru kaya masikini na utekelezaji wake yameandaliwa na mfuko wa maendeleo ya jamii tasaf yana laengo la kuwapa elimu masheha, walimu na maafisa wa afya ili kuweza kufahamu zaidi kazi yao.