SERIKALI KUENDELEA KUHESHIMU NA KUKUZA UHURU WA VYOMBO

 

Waziri wa habari wa habari utali na mambo ya kale mh mahamoud sabiti kombo amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar itaendelea kuheshimu na kukuza uhuru wa vyombo vya habari kama ilivyoelekeza katiba ya zanzibar ya mwaka 1984.

Amewataka waandishi wa habari kuzingatia uweledi, uzalendo,heshima kwa jamii na umuhimu wa kuwalinda wahusika na taaluma hiyo kwa umma.

Akizungumza na vyombo vya habari katika kuelekea maanzimosho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari amesema serikali inatambua umuhimu wa siku hiyo iliyotangazwa na baraza kuu la umoja wa mataifa mwaka 1993 kufuatia pendekezo la mkutano mkuu wa 26 wa unesco mwaka 1991 lililotokana na azimio la maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari.

Amesema wakati huu ikiwa dunia inaadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari hana budi kumshukuru  rais wa zanzbar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk ali mohamed shein kwa uamuzi wa kuviimarisha vyombo vya serikali na mageuzi ya kuijenga uwezo shirika la utangazaji zanzibar,

Ulimwengu unaadhimisha uhuru wa vyombo vya habari duniani maadhimisho ambayo yanafanyika kesho jijini accra ghana yakiongonzwa na shirika la elimu,sayansi na utamadumi la umoja wa mataifa unesco .