SERIKALI KUHAKIKISHA WANANCHI WAKE WANAISHI KWENYE MAZINGIRA MAZURI NA SALAMA

 

Mkuu wa wilaya magharib i’’ a’  ambae ni kaimu mkuu wa wilaya ya magharibi’’ b’’  captain  khatibu khamis mwadini, amesema serikali  itahakikisha wananchi wake wanaishi kwenye mazingira mazuri na salama .

Akikabidhi msaada wa vyakula na fedha kwa mwananchi alieathirika kwa  kuangukiwa na mnazi katika  paa la nyumba  huko  shehia ya fuoni  mnarani  captain khatib  amemtaka  mwananchi huyo kuwa na subra  katika kipindi hiki.

Hata hivyo amewaomba wananchi  wanaoishi katika maeneo yenye minazi na miti hatarishi ni vyema kuwasiliana na wafanyakazi wa idara ya misitu ili kuiondoa miti hiyo kabla ya kuleta madhara.

Akizungumza katika ziara hiyo sheha wa shehia ya mnarani ndugu ramadhani abdallah rajabu,amewashauri wananchi wa shehia hiyo kuwa waangalifu na kufuata utaratibu wa vibali katika idara ya misitu  ili  kuweza kupunguza miti hiyo.

Kwa upande wake mwananchi aliefikwa na  maafa hayo bi naifat  michael, ameishukuru serikali   kwa kumpatia  msaada.