SERIKALI KUIMARISHA HUDUMA MUHIMU MAENEO YA KIJIJINI

Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk ali mohammed shein amekitaka kituo cha utafiti wa kilimo kizimbani kukikuza kituo hicho kwa kuzalisha wataalamu wa kilimo ili kisaidia wananchi katika kukuza sekta ya kilimo.
Amesema serikali imekuwa ikiimarisha huduma muhimu maeneo ya kijijini ikiwemo miundombinu ya maji umeme na barabara ili kuwarahisishia shughuli za kilimo kuwa ajira vijijini.
Akizindua maonyesho ya kilimo huko dole kizimbani amesema kufanya hivyo ni kuunga mkono mpango wa serikali kuzalisha bidhaa za chakula cha kutosha na kupunguza uingizaji wa chakula kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wa uvamizi wa maeneo ya ardhi ya kilimo dk. Shein amezitaka taasisi zinazohusika na masuala ya ardhi kudhibiti maeneo ya kilimo kuvamiwa kwa shughuli za ujenzi inaharibu mipango ya serikali kuelekea mapinduzi ya kilimo.
Waziri wa kilimo maliasili mifugo na uvuvi mh. Hamad rashid amesema wakati umefika kwa vijana kutumia fursa zilizopo vijijini mwao ili kushiriki katika uzalishaji mali na kuacha kisingizio cha ukosefu wa kazi kwa kukimbilia mjini kusikowaletea tija.
Katibu mkuu wa wizara ya kilimo josef abdalla meza amesema wizara imejipanga kutoa taaluma kwa vijana kulima kilimo cha biashara ili wajikwamue na maisha.
Mapema dk shein alikagua maonyesho hayo ya kilimo ambayo ni ya kwanza kufanyika hapa nchini ambayo yatahusisha utoaji wa taaluma ya uzalishaji wa kilimo cha kisasa ikiwa ni maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayoadhimishwa ifikapo october 16 ya kila mwaka.