SERIKALI KULITAFUTIA UFUMBUZI TATIZO LA KUTOZWA KODI MARA MBILI

 

Wamiliki wa majahazi wameiomba serikalikulitafutia ufumbuzi tatizo la kutozwa kodi mara mbili wanapo kuwa katika kazi zao za usafirishaji  mizigo tanzania bara.

Wakizungumza  na zbc walipofka katka fukwe ya mazizini   mmoja wa  bahariai wa jahazi  ya hazina  abdala omar amesema wamekuwaWakipata tabu mara kwa mara wakati wakiwa katika shughuli zao za kazi na kuwaletea usumbufu  ikiwa pamoja na kulipia  mara mbili huduma ambayo wameshailipia zbar

Hata hivyo ameelezea changamoto wanazokumbana nazo wanapokuwa safarini katika kipindi cha mabadiliko  ya hali  ya hewa huku akiwataka wanaotumia usafiri wa majahazi kuacha tabia ya kusafirisha dawa za kulevya ambazo ni vita na serikali na kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi Zbc hata hivyo imeiona hali halisi ya uchafu wa fukwe hiyo  ambapo wananchi hawakutaka kusema chochote kuhusu hali hiyo na kuitupia lawama mamlaka husika.