SERIKALI KUMBOMOLEA ATAKAEJENGA KATIKA ENEO LISILOPATA RIDHAA YA TAASISI

 

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, ameonya na kusisitiza kwamba serikali haitamuonea huruma mtu yeyote atakaeamua kujenga nyumba au jengo lolote katika eneo lisilopata ridhaa ya taasisi inayohusika na masuala ya ujenzi, ardhi, mipango miji na vijiji.

Amesema hivi sasa kuna tabia ya muhali inayoendelea kufanywa na baadhi ya viongozi wanaopewa jukumu la kusimamia sheria na taratibu za serikali, kiasi kwamba watu huamua kuchukua sheria mikononi mwao.