SERIKALI KUPITIA SHIRIKA LA ZSTC KUZIDI KUTOWA MICHE YA KARAFUU

 

Wakulima wa karafuu na wadau wa zao hilo wameitaka serikali kupitia shirika la zstc kuzidi kutowa miche ya karafuu kwa wingi hasa katika kipindi cha mvua zinazoendelea kunyesha ilikukufikia malengo ya zao hilo hapa nchini.

Akisoma ripoti ya tathmini ya utekelezaji wa kazi kwa msimu wa mavuno ya karafuu kwa mwaka 2017- 18 katika mafvunzo iliyowakutanisha wakulima wa karafuu wa mkoa wa kusini  pamoja na wadau wa karafuu, katika  ukumbi wa skuli ya dunga mkurugenzi wa  mfuko wa maendeleo  zcts ali suleiman mussa amesema mashirikiano mazuri yaliyopo   yamesababisha kwa wakulima wengi kuitikia wito wa serikali kwa kuuza karafuu zaao zstc.

Amesema shirika litahakikisha kuwasaidia  wakulima na wafanya biashara wa zao hilo ili kuhakikisha malengo ya shirika hilo yanafanikiwa.

Nae mkuu wa mkoa wa kusini hassan khatib  amesema zao la karafuu linazidikupata  mafanikio  tangu serikali kuweka mikakati ya kuliokoa zao hilo hivyo amewataka wakulima pamoja na wadau wa karafuu kuongeza juhudi za kuboresha zao hilo ili kufanikisha malengo ya serikali.

Amewataka masheha na wananchi kuwafichuwa wanaouza mashamba kuwafichuwa huku akisema atakiunda kikosi kazi cha kuweza kufuatilia mashamba yote ya mkoa huo.

Kwa upande wao wakulima na wafanyabiashara wa zao hilo wamewalalamikia mikopo  pamoja na wafugaji kwa kutia mifugo yao katika shamba yao jambo ambalo linawarejesha nyuma juhudi zao .