SERIKALI KUPITISHA SHERIA YA UPATIKANAJI WA TAARIFA

Serikali imeombwa kuanza hatua ya majadiliano ya kuandaa kanuni zitakazotumika katika sheria ya upatikanaji wa taarifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar-es-salaam, mwenyekiti wa umoja wa haki ya kupata taarifa ndugu kajubi mukajanga amesema japokuwa serikali imepitisha sheria ya upatikanaji wa habari bado sheria hiyo haijaundiwa kanuni zinazoiratibu.
Aidha ndugu mukajanga amesema kwa mara nyingine asasi hiyo inaipongeza serikali kwa kupitisha sheria ya upatikanaji wa taarifa hususan kwa kuthamini mawazo na maoni ya baadhi ya wadau kabla ya sheria hiyo haijapitishwa.
naye meneja utetezi wa asasi ya twaweza bi anastazia lugaba ameelezea changamoto zilizopo katika utoaji wa taarifa kwenye ofisi za umma.
Siku ya kimataifa ya upatikanaji wa taarifa huadhimishwa duniani kila ifikapo tarehe 28 ya mwezi september , na ilianzwa kuazimishwa mwaka 2003