SERIKALI KUTENGA ASLIMIA 30 YA MAPATO YA UKODISHAJI MASHAMBA

Serikali imesema imemau kutenga aslimia 30 ya mapato ya ukodishaji mashamba inayoyamiliki ili kuyaimarisha kutokana na kukaa katika hali isiyoridhisha kwa muda mrefu.
Waziri wa kilimo maliasili mifugo na uvuvi mh. Hamadi rashid amesema mashamba hayo yameendelea kuwa na pori kutokana na uhaba wa wafanyakazi pamoja na fedha baada ya zile zinazolipwa kwa ukodishaji zinapelekwa moja kwa moja hazina.
Akijibu swali katika baraza la wawakilishi amesema mashamba hayo yanaendelea kuwa na pori kutokana na kukosa huduma ya usafi kutoakana na ukosefu wa wafanyakazi na uhaba wa fedha kwa vile fedha zote za ukodishwaji zinapelekwa hazina.
Waziri rashid amefahamisha kuwa mbali na fedha hizo kutumika kwa ajili ya kazi hiyo pia zitatumika katika upandaji wa mazo mengine na elimu kwa wakulima.
Akizungumzia kuhusu mapato ya ukusanyaji wa mashamba ya mikarafuu amesema wamekuwa wakikusanya zaidi ya shilingi milioni mia moja kwa shamba la makuwe kwa mwaka 2014 hadi 2015 na kiasi cha shilingi milioni kumi na tisa laki nne kwa shamba la kinyasini imekusanya katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2016,
Wakati huo huo naibu waziri wa nchi ofisi ya rais katiba sheria utumishi wa umma na utawala bora, mh. Khamis juma mwalimu amesema ofisi ya mkaguzi mkuu wa serikali imekuwa ikaguliwa na shirika la taifa la ukaguzi la tanzania (tac) ili kujihakiki utendaji wake.