SERIKALI KUVUNJA NYUMBA ZOTE ZILIZOJENGWA KATIKA VIWANJA VYA WATU

 

 

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo na makazi mh. William lukuvi amesema serikali itazivunja nyumba zote zilizojengwa katika viwanja vya watu na wavamizi wa maeneo.

 waziri lukuvi ametangaza uamuzi huo wakati akitatua migogoro ya ardhi kwa wakazi wa jiji la dar es salaam pamoja na wananchi hao kuwataja matapeli wa ardhi ambapo amesema zoezi la uvunjaji wa nyumba litaanza wiki ijayo katika jiji hilo.

Aidha waziri lukuvi amesema katika kuhakikisha wizara yake inamaliza migogoro ya ardhi nchini wizara imeanzisha kampeni ijulikanayo kwa jina la funguka na waziri lukuvi ikiwa na lengo la kutatua migogoro ya ardhi huku akiwataka wananchi kuwataja matapeli wa ardhi nchini.

Uamuzi huo wa mh waziri ulitokana na malalamiko ya wananchi wengi yaliyowasilishwa hapo awali ambayo yalikua ni kuvamiwa kwa maeneo yao.

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi wiliam lukuvi yupo katika jiji la dar es salaam akiwa na lengo la kutatua migogoro ya ardhi katika jiji hilo ambalo limetajwa kuongoza kwa migogoro ya ardhi.