SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATU WANAOJIHUSISHA NA MAGENDO YA KARAFUU

Serikali imesema itaendelea kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na magendo ya karafuu ambayo yanaharibu haiba na hadhi ya zao hilo kimataifa.
Waziri wa biashara viwanda na masoko balozi amina salum ali amesema sheria ya magendo ya karafuu iliyofanyiwa marekebisho imeshaanza kutumia hivyo mwanachi yoyote atakae kamatwa na karafuu katika maeneo yasiyokubalika atachukuliwa hatua za kisheria, kwani tatizo hilo ni sugu kwa baadhi ya wananchi jambo ambalo linakosesha serikali fedha za kigeni.
Balozi amina ametowa kauli hiyo mjimbini kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa uchumaji wa karafuu kwa mwaka 2017 – 2018 pamoja na kuzindua kituo cha kununulia karafuu mjimbini kilichogharimu shilingi milioni 56 katika ukarabati wake.
Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa kusini pemba mh. Mwanajuma majid abdalla na mkoa wa kaskazini pemba mh. Omar khamis othman kwa pamoja wapiga marufuku uokotaji wa mpeta na kukataza watoto kushirikishwa katika uchumaji wa karafuu.
Katibu mkuu wizara ya biashara viwanda na masoko bakar haji na mkurugenzi muendeshaji wa zstc said seif wamewataka wananchi kuunga mkono juhudi za serikali za kuzifanya karafuu kuwa ni zao la biashara la kuoneza ubora wa maisha waliyonayo.