SERIKALI MTANDAO NI MPANGO ULIOLENGA KURAHISISHA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Utumiaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano “serikali mtandao”  ni mpango uliolenga kuimarisha ufanisi, na utoaji huduma bora na urahisi kwa wananchi kupitia taasisi za serikali na umma.

hayo yameelezwa na mkurugenzi wa serikali mtandao e’government ndugu shabaan haji chum katika utoaji wa mafunzo kwa kamati ya sheria, utawala bora na idara maalum ya baraza la wawakilishi, yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali iliyopo mazizini, unguja.

amesema lengo la mafunzo hayo ni kueneza dhana ya serikali mtandao kwa jamii, na elimu kwa  kamati hiyo ni njia moja wapo ya kuwafikishia wananchi kupitia wajumbe wao wa baraza la  wawakilishi.

waziri wa katiba sheria, utumishi wa umma na utawala bora mhe. Haroun ali suleiman amesema juhudi lazima ziongezwe katika utoaji elimu ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi.

 

Mwenyekiti wa kamati ya sheria, utawala bora na idara maalum mhe. Machano othman said amesema  kutokana na umuhimu serikali mtandao ni vyema idara hiyo kuwa wakala wa serikali  ili kufanya kazi zake kwa uweledi zaidi.

 

Wajumbe wa kamati hiyo walipata fursa ya kuchangia maoni na ushauri ili kuhakikisha ufanisi katika lengo  lakuanzishwa kwake linafikiwa.