SERIKALI WA KUJENGA MAJENGO YA KISASA YA BIASHARA

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dk Ali Mohd Shein amesema mpango wa serikali wa kujenga majengo ya kisasa ya biashara na makaazi ni mpango endelevu ambao manufaa yake ni makubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

Amesema kwa kutambua fursa hiyo ni vyema kwa wafanyabiashara watakaobahatika kuweka vitega uchumi katika jengo la treni darajani ambalo limezinduliwa kuhakikisha wanalitunza kwa faida ya wananachi na serikali.

Amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar imeamua kujenga maduka ya kisasa ili kila mwananchi afanye biashara katika mazingira mazuri na yaliyo bora   katika hali ya usafi.

Dk shein ametoa agizo hilo katika hafla ya uzinduzi wa jengo la  vitega uchumi darajani mjini unguja ambalolimefanyiwa matengenezo makubwa baada ya kuonekana kuwa hatari na tishio kwa maisha ya wakaazi na wafanya biashara waliokuwepo awali.

Uzniduzi huo ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 20 ya zssf ambapo dk. Shein amesema historia ya mji wa darajani ni ya muda mrefu hasa kupitia  biashara  katika ukanda wa afrika mashariki hivyo ikiwa jengo hilo litatunzwa  kwa kuwekwa katika hali ya unadhifu  litakuwa kielelezo cha mji wa zanzibar kwa kuwavutia wenyeji na  wageni wanaotembelea  mji huo..

Dk shein amesema uamuzi wa serikali wa kujenga majengo ya kisasa ya kibiashara katika manisapaa ya mji wa zanzibar ni endelevu kwani wahisani wanaendelea kuiunga mkono serikali ili kuleta mabadiliko.

waziri wa fedha na mipango dk. Khalid salum mohd amesema kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo la biashara utakwenda sambamba na ujenzi wa maeneo mengine ikiwa lengo la serikali la kuimarisha  makaazi  ya wananchi.

Mkurugenzi mwandeshaji wa mfuko wa hifadhi ya jamii zanzibar ndugu sabra issa machano ameelezea mikakati ya mfuko ni kuendeleza majengo iliyoyaanzisha na miradi mipya ikiwemo ya makaazi katika eneo la kwahani na chumbuni.

Jengo  la kufanyia biashara lililokuwepo maeneo ya darajani lilijengwa mnamo miaka 1888 chini  ya utawala wa said barghash kwa sasa litakuwa na uwezo wa kuchukuwa zaidi ya wafanyabiashara 52 na mikahawa, , kumbi za mikutano pamoja na huduma za kibenki (atm).