SERIKALI WILAYA YA KUSINI IMEPIGA MARUFUKU UTUMIAJI WA BWACHI KATIKA ENEO LA UFUGAJI WA PWEZA MTENDE

Serikali ya wilaya ya kusini imepiga marufuku utumiaji wa bwachi katika eneo la linalotumika kwa ufugaji wa pweza huko mtende hadi watakapoangalia sheria za idara ya uvuvi.
Mkuu wa wilaya ya kusini unguja nd. Idrissa kitwana ametoa agizo hilo kufuatia wavuvi wa mtende kufuga pweza bila ya kufuata sheria za idara ya uvuvi na kusababisha kutokea kwa migogoro kati ya wavuvi wa kijiji hicho na wavuvi wa mzuri.
Amesema wameamua kufanya hivyo ili kuondosha migogoro iliyopo kati ya wavuvi wa mtende na mzuri,na kuhakikisha sekta ya uvuvi inaendelea na kukua kwa maslahi ya wavuvi na taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi idara ya maendeleo ya uvuvi mussa aboud jumbe akitolea ufafanuzi juu ya tatizo hilo katika kikao cha pamoja na wenyeviti wa uvuvi,amesema kwa mujibu wa sheria na kanuni za idara hakuna taarifa kwa mvuvi yoyote kufuga pweza na wavuvi wa mtende kuamua ,hivyo idara imewataka kufuata taratibu za kisheria ili kuepuka migogoro.
Kwa upande wao wenyeviti wa kamati za uvuvi za mtene na mzuri wamesema uamuzi uliotolewa na serikali wa kutolitumia eneo hilo kwa shughuli yoyote ya uvuvi ni mzuri na utaweza kuepusha migogoro kati yao.