SERIKALI YA AWAMU YA TANO INAENDELEA NA KASI YA KUSHUGHULIKIA MIUNDO MBINU YA BARABARA

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi mh. Hamadi yusuph masauni amesema gari zitakazobandikwa stika kipindi cha kuelekea wiki ya usalama barabarani ni zile zitakazofanyiwa ukaguzi tu.
Naibu waziri masauni ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la taifa la usalama barabarani ameyasema hayo wakati wa kikao cha pamoja na wafadhili wa sherehe za wiki ya usalama barabarani.
Amesema jumla ya wakaguzi 300 watakuwapo nchi nzima ambapo hatua ya kwanza itahusisha magari ya abiria na magari yanayobeba wanafunzi.
naye naibu waziri wa ujenzi ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa baraza hilo mhe elias kwandikwa amesema serikali ya awamu ya tano itaendelea na kasi ya kushughulikia miundo mbinu ya barabara kwa kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya mazingira ya barabara na suala la ajali za barabarani.
Maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani yanatarajiwa kufanyika mkoani kilimanjaro.