SERIKALI YA JAMUHURI YA WATU WA CHINA IMESEMA ITAENDELEA KUISAIDIA SMZ

 

Serikali ya jamuhuri ya watu wa china imesema itaendelea kuisaidia serikal ya mapinduzi ya zanzibar katika kuwapatia mafunzo ya muda mfupi na mrefu  wafanyakazi wake  kwa lengo la kujiengezea ufanisi katika utendaji wao wa kazi.

Kauli hiyo imetolewa na balozi mdogo wa china mr xie xiaowu katika hafla ya kuwaaga wanafunzi 35 wa fani mbalimbali za uchumi, afya na nyenginezo waliobahatika kupata nafasi ya kwenda nchini china kwa masomo ya muda mrefu.

Balozi xie amewataka wanafunzi hao kutumia vizuri nafasi waliyoipata  kwani watu wengi waliomba nafasi  hiyo hawakubahatika.

Nao wanafunzi waliobahatika kupata nafasi hiyo wameishukuru serikali ya mapindzu ya zanzibar kwa kuweza kuwapatia nafasi ya kuweza kujiendele na kuahidi kuitumia nafasi hiyo kama walivyo kusudia  na kuisaidaia nchi kupata maendeleao.

Jumla ya wanafunzi 29 kutoka wizara mbali mbali wanatarajiwa kuondoka wiki ijayo kwenda nchini china kwa ajili ya masomo.