SERIKALI YA MAPINDUZI IMEAMUA KUIUZA MELI YA ABIRIA NA MIZIGO MV MAENDELEO NA MT MKOMBOZI

Serikali   ya  mapinduzi  ya  zanzibar  imeamua  kuiuza  meli  ya  abiria na mizigo mv maendeleo  na  mt  mkombozi  ya kubebea mafuta kutokana  na  uchakavu.

Hali  hiyo  italipunguzia  mzigo  shirika  la  meli  kutokana  na  uwendeshaji  wa  shirika  na  kufuata  maelekezo  ya  shirika  linalosimamia  maswala  ya  meli  duniani imo.

Akijibu  swali  katika  kikao  cha  baraza  la  wawakilishi  naibu  waziri  wa ujenzi  miundombinu  na  usafirishaji mh; moh’d  ahmada  salum  amesema  tangazo  rasmi  la  kuuzwa  kwa   meli  hizo litatoka  mara tu  baada  ya  utaratibu  husika  litakapokamilika.

Amefahamisha  kuwa  kwa  sasa   meli  ya  mt  mkombozi  imepoteza  sifa  ya  kufanya  biashara  kutokana  na  maumbile  yake.                                                                    

Mh’ ah’mada  amesema  katika  kuimarisha  huduma  za  usafiri wa  bahari  na  kukuwa  kwa  huduma  za  kijamii, kiuchumi, na kibiashara  serikali  imenunua  meli  mpya  za  kisasa  mv  mapinduzi 11 ambapo  hivi  sasa  serikali  inakamilisha  taratibu  za ujenzi  kwa  meli  mpya  za  abiria  na  mizigo  pamoja  na  meli  ya  mafuta  ili  kukuza  huduma  hizo zaid.

 meli  ya  mv maendeleo  na  mt mkombozi  zimenunuliwa  mwaka  1980  na  serikali ya  mapinduzi  ya  zanzibar  zikiwa  mpya  nchini   japan.