SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEJIPANGA KUIMARISHA MIJI MIPYA

 

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuimarisha miji mipya katika mikoa yote ya zanzibar ili kusaidia kuondosha msongomano katika mkoa wa mjini magharibi ambao idadi ya wakaazi wake ni wengi hivyo kufanya mahitaji ya mji huo kuwa makubwa.

Taarifa ya khadija khamis inasomwa na nassra khatib

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002 idadi ya watu katika mkoa huo ilkuwa ni zaidi ya laki tano na elfu thamanini na nne ikiwa ni asilimia 44. 9 ya wakaazi wote wa zanzibar ambapo inakadiriwa ifikapo 2020 idadi itaongezeka na kufikia laki saba na elfu 33.

Waziri wa fedha na mipango Dk. Khalid Salum Mohamed akijibu maswali ya wajumbe wa baraza la wawakilishi amesema kwa takwimu hiyo serikali ishafikiria kupanua miji mipya katika eneo la mahonda na chwaka pamoja na kuhakikisha kuwa mahitaji yote muhimu yanapatikana katika miji hiyo ili kuepuka wimbi la watu kukimbilia mkoa wa mjini magharibi kutafuta fursa mbalimbali.

Wakati huo huo wizara ya afya imesema serikali imeshatenga shilingi bilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa mashine ya DNA na hatua za manunuzi zinaendelea ila kuchelewa kwake kunatokana na kufuatwa taratibu za kisheria zilizopo ikiwemo hatua za kiusalama ili kukamilisha ununuzi huo.