SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMETANGAZA BEI YA MCHANGA

Serikali ya mapinduzi  ya zanzibar  imetangaza bei ya

Mchanga  ambayo itatumika  katika kituo cha kuuzia

Bidhaa hiyo mwanakwerekwe.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari waziri wa  kilimo , mliasili, mifugo na uvuvi mhe, hamad  rashid mohammed  amesema bei hizo zinafuatia serikali kuweka utaratibu mzuri  wa kuvuna na kutumia rasilimali hiyo inayoonekana kupungua kila kukicha kutokana na mahitaji kuwa makubwa.

Waziri  ametaja bei hizo kuwa  tani 15 za mchanga  zitauzwa sh. 300,000/, tani 10 sh.220,000,tani saba 7 shilingi 150,000, tani nne sh. 100,000,wakati  tani 2 zitauzwa shilingi 70,000 katika soko hilo.

Mh,  hamadi amewataka wafanyabiashira wa mchanga kufuata utaratibu huo huku akionya watakaokwenda  kinyume watachukuliwa kisheria ikiwemo  kulipa faini ya shilingi  milioni tatu.