SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUYAFANYIA MATENGENEZO MAGOFU YA MKAMANDUME PUJINI

 

katibu mkuu wizara ya habari, utalii na mambo ya kale, bi khadija bakar juma amesema hatua ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar kuyafanyia matengenezo magofu ya mkamandume pujini ina lengo kuendeleza historia yake pamoja na kuvutia wageni.

amesema hatua hiyo itatoa taswira halisi ya eneo hilo na wageni wataweza kuona ngome ya mkamandume na sio kupata maelezo pekee.

katibu khadija amesema hayo wakati akijibu masuali yaliyoulizwa na wajumbe wa kamati ya habari maendeleo ya wanawake na utalii ya blm chini ya mwenyekiti wake mh. mwantatu mbaraka khamis baada ya kutembelea na kupata taarifa ya matengenezo ya eneo hilo kutoka kwa mhandisi ali mbarouk aliyekabidhiwa kazi hiyo.

mapema wajumbe wa kamati hiyo walipokea taarifa ya utekelezaji kazi wa idara ya makumbusho na mambo ya kale pamoja na kamisheni ya utalii.

katika ziara hiyo ya kukagua utekelezaji kazi wa robo mwaka 2018 – 2019 wajumbe wa kamati ya habari maendeleo ya wanawake na utalii ya blm, wametembelea makumbusho ya chake chake, hotel ya sun seat wesha na magofu ya jambang’ome.

akielezea matengenezo hayo mhandisi wa mradi huo ali mbarouk amesema utajumuisha ujenzi wa kuta tatu, uchimbaji wa kisima cha wivu, ngazi na umtaro ambao akiutumia mkamandume katika safari zake.