SERIKALI YA MKOA WA MJINI MAGHARIBI IMEFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI

 

Serikali ya mkoa wa mjini magharibi imefungua milango ya uwekezaji kwa kampuni  ya Inter Capital Limited ya Dar-es-Salaam inayohusika na ujenzi wa majengo ya kibiashara utiaji  thamani wa miradi mbali mbali ya uwekezaji  ili kuongeza kasi ya ukuwaji wa kiuchumi katika ngazi ya Mkoa na Serikali za Mitaa.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud ameeleza hayo katika kikao maalum cha majadiliano  na uongozi wa kampuni hiyo hapo ofisini kwake Vuga uliofika kufuatia mazungumzo ya awali yaliyofanyika Mkoa wa Dar-es-salam wiki iliyopita  ulioshirikisha viongozi mbali mbali wa Mkoa, Mabaraza ya Manispaa,Wilaya na wataalam wa kutoka Idara ya mipango miji na vijiji,Idara ya Mazingira na Mkurugenzi Idara ya Ujenzi.

Amesema mahusiano waliyoyaanzisha yatatoa  fursa mbali mbali za uwekezaji katika uendelezaji wa    majengo ya taasisi za Serikali na ya  kibiashara   na kuleta tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Akiwasilisha  Michoro ya ramani ya mradi wa maendeleo  ya Darajani Koridoo katika kikao hicho Mwenyekiti wa mradi huo Nd Yassir De Costa  amesema  malengo ya serikali ni kuliendeleza eneo la darajani kuwa na majengo a kisasa ya biashara ambapo  michoro ya ramani  imeshawasilishwa serikalini   na kampuni ya PHILLS INTERNATIONAL  kutoka nchini Dubai  katika na  imezingatia vigezo vyote vya urithi wa kimataifa.

Nae Afisa mipango miji ndugu Muchi Juma Ameir ambae aliwasilisha mradi wa uendelezaji wa  wa maeneo ya wazi yakiwemo bustani ya Kiembesamaki na viwanja vya kibanda maiti amesema serikali inalengo la kupunguza msongamano katika upatikanaji wa huduma za kijamii na maeneo ya kupumzikia  katika Manispaa ya Mji.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Inter Capital Limited Nd Anthony  Chamungwana  amesema kampuni yake  , itahakikisha inatumia fursa zilizopo katika maeneo ya manispaa za Mkoa wa mjini magharibi  ili   kuleta mabadiliko na kuimarisha miundombinu hasa ya majengo kwenye Mkoa huo.

Wajumbe wa mkuano huo walitembelea Maeneo ya  yaliyopendekezwa kwa ajili ya uwekezaji ikiwemo eneo la  Darajani ,eneo la kituo cha daladala kijangwani eneo la kiwanja cha ofisi ya Mkuu wa Mkoa  ,Amani  soko la saateni, eneo la wafanyabiashara kwa Wilaya ya Mjini na eneo la ujenzi wa Bustani ya kiembesamaki  na Chuini lililotengwa na serikali kwa ajili ya uwekezaji .