SERIKALI YA SYRIA NA WAASI WAMEFANYA UHALIFU ALEPPO

Wachunguzi wa umoja wa mataifa wamesema pande zote mbili zimefanya uhalifu wa kivita katika mzozo wa aleppo nchini syria ikiwa ni pamoja na majeshi ya nchi hiyo kutumia ndege kuulipua msafara wa kutoa misaada.
Ripoti iliyotolewa na un imesema majeshi ya syria na urusi yalifanya mashambulizi ya angani katika mji unaodhibitiwa na waasi wa aleppo kati ya mwezi julai na desemba, na kuwaua mamia ya watu na kuharibu miundombinu ya mji huo.
Waasi wanashutumiwa kwa kuwatumia raia kama ngao magharibi mwa aleppo