SERIKALI YA TUNISIA IMETANGAZA AZMA YA KUZIDISHA MISAADA KWA WATU WASIOJIMUDU.

 

 

Serikali ya tunisia imetangaza azma ya kuzidisha misaada kwa  watu wasiojimudu.Uamuzi huo umepitishwa kufuatia wimbi la maandamano na machafuko dhidi ya kupanda kwa bei za vitu na kodi za mapato.Waziri wa masuala ya jamii mohammed trabelsi amesema misaada ya jamii itaongezeka hadi kufikia euro milioni 60.familia zisizopungua laki mbili na nusu zitafaidika na mpango huo.

Wimbi la maandamano lilienea kote nchini tunisia na kuangamiza maisha ya mtu mmoja ambapo serikali ilituma wanajeshi kuwadhibiti waandamanaji na kiasi ya wanaharakati 800 wamekamatwa.