SERIKALI YATAKIWA KUFANYA UTAFITI KUHUSU TATIZO LA MITI YA MIKOKO KUSHINDWA KUSTAWI

Wakaazi wa kijiji cha muwanda wameomba kupatiwa wataalamu zaidi watakaofanya utafiti juu ya tatizo linalosababisha mikoko kushindwa kustawi katika kijiji hicho.
Wakizungumza katika upandaji miti katika eneo la fukwe la kijiji hicho baadhi ya wanaharakati wa mazingira wamesema mara nyingi wanapopanda miti hiyo inashindwa kustawi na hawafahamu sababu inayochangia kuendelea hali hiyo.
Mratibu wa mikoko idara ya misitu na mali zisizorejesheka zanzibar ameir himid ali amesema tatizo hilo la kukauka kwa mikoko linasababishwa na wadudu wanaoharibu miti hiyo na sasa wanaendelea kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.
Mwenyekiti wa jumuiya ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi zanzibar (zacca) amina yussuf kasholo amesema wamepanga kuendeleza juhudi za upandaji miti ya mikoko ilikuhakikisha maeneo ya ukanda wa pwani ili kunusuru athari za kutokea jangwa pamoja na kuongezeka kina cha bahari katika maeneo ya makaazi.
Jumuiya hiyo katika hatua ya awali imepanda mikoko zaidi ya elfu tatu katika pwani ya kijiji hicho cha muwanda kupitia mradi wa kuwawezesha wanavijini kukabiliana na uharibifu mazingira unaofadhiliwa na taasisi ya piscca kutoka ufaransa.