SERIKALI ZINAWASHAJIHISHA WAZEE NA KUWEZA KUPATA FURSA MBALIMBALI ZA KIMAISHA

Wazee wanaoishi nyumba za serikali za sebleni na welezo wameishukuru serikali ya mapinduzi zanzibar kwa kuendelea na dhamira ya hayati mzee abeid amani karume, ya kuwaenzi, kuwathamini na kuwapatia fursa mbalimbali za kimaisha.
Wakizungumza katika ziara ya kubadilisha mazingira huko forodhani, wamesema serikali za awamu zote zinawashajihisha wazee na kuweza kupata fursa mbalimbali za kimaisha ikiwemo hiyo ya kutembelea maeneo ya burudani.
Wamesema wamefarajika kufika maeneo hayo na kujihisi wanaenziwa na kuthaminiwa kutokana na muda mrefu kutofika katika mazingira kama hayo.
Baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wamefurahishwa na utaratibu huo na kushauri uwe endelevu.
Mkuu wa nyumba za wazee sebleni ashura suleiman juma, amesema wameamua kuwatembeza wazee hao baada ya kumaliza funga ya sita ikiwa ni miongoni mwa sikukuu kwao.