SERIKLALI KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI UTAKAPOANZA

 

 

 

Seriklali ya Mapinduzi ya Zanzibar   imesema itahakikisha  inakabiliana  na uharibifu wa mazingira pindi zoezi la uchimbaji wa mafuta na gesi  utakapoanza nchini.

Naibu waziri wizara ya ardhi maji nishati na mazingira mh. Juma makungu akifungua mafunzo kwa wadau wa kimazingira kutoka nchi kumi za afrika mashariki , amesema zanzibar ipo katika harakati za  utafiti wa uchimbaji wa mafuta na gesi hivyo mafunzo hayo yatasaidia juu ya kukabiliana na athari  zitakazojitokeza hasa katka miundo mbinu ya bahari.

Akijibu swali kwa waandishi wa habari juu ya utowaji wa taarifa ya utafiti wa uchimbaji wa mafuta mh. Makungu  amesema kwa sasa serikali haiwezi kutoa taarifa ya pahala husika yatakapochimbwa mafuta hayo kwani muda uliotakiwa kutolewa taarifa na watafiti juu ya uchimbaji huo bado haujafikia .

Mkurugenzi wa mamlaka ya mazingira ndugu sheha mjaja juma, amesema  iwapo zanzibar haijajipanga mapema katika masuala ya kimazingira  kunaweza kutokea athari kubwa ambayo itaweza kuathiri shughuli za  kijamii,kiuchumi,kimazingira na kiutalii.

Nd.mjaja amesema asilimia 90 ya wananchi wa zanzibar wanategemea bahari kwa ajili ya shughuli zao mbali mbali za kila siku , hivyo ni vyema kuisimami miundo mbinu hiyo ili isiweze kuharibika, na kuwataka  wananchi kuondoa  wasiwasi pindi zoezi hilo litaakapoanza  kwani litafanywa kwa usalama  bila ya kutokea athari yoyote.

Mkutano huo wa siku nne  ambao umezishirikisha nchi kumi za afrika ikiwemo comoro,kenya,madagascar,mauritius,mozimbique,seychelles,somalia, afrika ya kusini, tanzania na uganda  una lengo la kutoa elimu juu ya  kukabilina na athari za kimazingira  katika uchimbaji wa mafuta na gesi.