SHAMBULIIO LA KIGAIDI MJINI KABUL LAANGAMIZA MAISHAB YA WATU WASIOPUNGUA 11

 

 

Watu wasiopungua 11 wameuwawa kufuatia shambulio la kigaidi katika mji mkuu wa Afghanistan-Kabul. Kwa mujibu wa vyombo vya habari, mtu mmoja amejiripua alipokuwa karibu na vikosi vya usalama na umati wa watu waliokuwa wakiandamana.Yadhihirika waandamanaji pia ni miongoni mwa wahanga wa shambulio hilo. Waandamanaji hao walikuwa wakilalamika dhidi ya kifo cha tajiri mmoja, polisi walipokuwa wakifanya msako dhidi ya biashara haramu ya vinywaji vikali na madawa ya kulevya. Mshambuliaji anasemekana alivaa sare za polisi alipoingia katikati ya mji mkuu Kabul na kujiripua. Magaidi wanaojiita wa dini ya kiislam-IS, wanadai kuhusika na shambulio hilo.