SHEHIA YA KIFUNDI WAMEPOGEZA SERIKALI KUTAKA KUWAJENGEA KITUO CHA AFYA

 

Wananchi wa kijiji cha kipangani shehia ya kifundi wamepogeza uwamuzi wa serikali wa kutaka kuwajengeakituo cha afya cha daraja la pili katika kijiji chao na kwamba kitawapunguzia usumbufu wa kufuata huduma za mama na mtoto katika kituo cha afya cha konde.

Akizunghumza na zbc kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho ramadhan yusuf  amesema kujengwa kwa kituo hicho kitaondosha usumbufu wa kuzifuata huduma za afya hasa wanapotokea mama mjamzito anapotaka kujifungua.

Yusuf ametowa pongezi hizo baada ya uongozi wa serikali ya mkoa wa kaskazini pemba kutembelea na kukagua eneo ambalo linatarajiwa kujengwa kituo hicho katika kijiji cha kipangani wilaya ya micheweni.

Naye katibu tawala mkoa wa kaskazini pemba ahmed khalid abdalla amesema  ujenzi wa kituo hicho itakuwa ni ukombozi wa wananchi wa kijiji hicho kwani kituo cha afya za sasa hakitoshelezi mahitaji ya wananchi .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya micheweni salama mbarouk khatiba na afisa mdhamini wizara ya afya bakari ali bakar meiyomba  halmashauri ya wilaya ya micheweni kusimamia upimaji wa eneo hilo ili  maeneo yatakayobaki yatumike kwa shughuli nyengine za kijamii.