SHERIA INAYOHUSIANA NA VITENDO VYA UDHALILISHAJI

 

Umoja wa wanawake wa wilaya mfenesini wameomba   sheria inayohusiana na vitendo vya udhalilishaji kuanza utekelezaji wake ili kukomesha vitendo hivyo.

Wakitoa  michango yao  katika  kongamano  la shamra shamra ya  kuadhimisha  siku ya  wanawake duniani wamesema   umefika  wakati  wa  kufanyiwa  kazi  mswaada  wa  sheria  hiyo kiuhalisia  ili  kuweza kuvikomesha  vitendo  hivyo vinavyolenga kuviteketeza  vizazi ambavyo  ni  taifa la kesho.

Wamefahamisha kuwa   hatua  ya  utekelezaji  wa  sheria  hiyo  itawezesha walau   kuiacha jamii  katika  mazingira  salama .

Mgeni  rasmin  katika  kongamano  hilo mwakilishi  wa  jimbo  la  kijitoupele  mh  ali  suleiman shihata  amesisitiza  wazazi  na  walezi  kuacha  kumalizana  kienyeji katka kesi  za  udhalilishaji  ili  kuvikomesha  vitendo  hivyo  katika  jamii.