SHILINGI BILION KUMI NA SABA NUKTA NANE SABA ZIMETUMIKA KATIKA UJENZI WA MSIKITI

 

Zaidi ya  shilingi bilion kumi na saba nukta  nane saba  zimetumika  katika ujenzi wa msikiti  uliopo  chuo cha kiislamu  kiembe samaki  mjini zanzibar

Akizungumza katika hafla ya kukutana na viongozi  wa wizara ya  elimu  baloz mdogo wa omani aliopo zanzibar  nd hamoud al-haps amesema ujio  wake  una lengo la kuimarisha na kuiendeleza sekta ya elimu  kwa kuinua taaluma  na vipaji  vya wanafunzi kwa kuwashauri viongozi wa wizara hiyo  kuufungua msikiti huo  ambao  utajumuisha  shughuli za ibada pamoja na utoaji  wa taaluma  mbali mbali akitoa shukrani  kwa ujio huo waziri wa elimu na mafunzo ya amali mh riziki  pembe  juma ameahidi kuwa pamoja na washirika hao  wa maendeleo katika kuhakikisha  msikiti huo unafunguliwa na unatumika  kwa lengo lililokusudiwa la kuongeza wataalamu  bora inchini

Naibu katibu mkuu utawala   mw abdallah  mzee amesema msikiti huo  wa kisasa na unasehemu  mbili za kusalia  wanawake na wanaume  nyumba sita  vya kusomea  maabara  na vyumba vya compyuter  umejengwa ukiwa chini ya kampuni  ya estem contructionya daresalamu  kwa ufadhili wa  inchi ya omani  na utatumiwa na zaidi ya elfu nne kwa wakati