SHINZO ABE AMEPATA USHINDI MKUBWA KATIKA UCHAGUZI ULIOITISHWA HARAKA

 

Waziri mkuu wa japan, shinzo abe amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi ulioitishwa haraka, na mara moja akaahidi kushughulikia kwa nguvu vitisho kutoka korea kaskazini, ambavyo vilikuwa mada kuu katika kampeni za uchaguzi huo.

Muungano wa abe unaotawala wa vyama vya kihafidhina ulikuwa unatazamiwa kushinda viti 310 kati ya viti 465 vya bunge.

Hii itampa waziri mkuu wingi mkubwa wa theluthi mbili, na kumruhusu kupendekeza mabadiliko katika katiba ya japan iliyolazimishwa na marekani baada ya vita vikuu vya dunia, ambayo inailaazimisha kutojihusisha na vita, na kudhibiti jukumu lake la kijeshi la kujihami.