SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR, LIMETANGAZA KUFUTA NAFASI ZA AJIRA MIA MBILI KWA KUJITOLEA

Shirika la Bandari  Zanzibar, limetangaza kufuta nafasi za ajira kwa wafanyakazi zaidi ya mia mbili wa kujitolea katika vitengo tofauti bandarini hapo.

hatua hiyo imefanyika baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya serikali, shirika la bandari na bodi ya shirika hilo kutokana na wingi wa wafanyakazi hao ikilinganishwa na uwezo wa shirika.

mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo Salmini Senga salmini, akizungumza na wafanyakazi hao wa kundi c,  amesema hatua hiyo haina lengo la kuwaadhibu bali, inajali maslahi ya pande zote mbili.

amesema idadi kamili ya wafanyakazi wanaojitolea na kulipwa kwa mkataba ni zaidi ya mia tano lakini watu mia tatu na 16 wataingia katika mchakato wa ajira kwa kuzingatia sifa na vigezo vinavyohitajika.

Mkurugenzi Mkuu shirika la bandari Zanzibar, Abdalla Juma Abdalla, amesema mbali na hatua hiyo shirika limejitolea kuwalipa kiasi cha fedha kwa muda waliolitumikia.

kwa upande wa wafanyakazi wameelezea maoni tofauti kuhusiana na hatua hiyo itakayoanza kutekelezwa kuanzia kesho.