SHIRIKA LA UMEME ZANZIBAR ZECO LAIMARISHA HUDUMA

 

 

shirika la umeme zanzibar zeco limesema katika kuhakikisha linaimarisha huduma za umeme, limejipanga kuona vikwazo mbalimbali vinaondoka ikiwemo kutatua uhaba wa usafiri ili kufikisha huduma kwa wakati.

meneja wa zeco akizungumza katika uzinduzi wa gari saba kwa ajili ya shughuli za shirika hilo amesema baadhi ya wakati tatizo la usafiri lilikuwa likisababisha kukwamisha kazi za shirika lakini kupitia gari hizo zitasaidia kuimarisha utoaji wa huduma.

amesema zeco imejipangia mikakati mingi akizindua gari hizo zilizogharimu shilingi milioni mia tatu mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi shirika la umeme shafi mussa amesema ni jukumu la watendaji kuhakikisha gari hizo zinatunzwa kwa faida ya shirika na wananchi katika kupata huduma za uhakika hasa inapotokea dharura.