SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI GREEN LIGHT FOUNDATION LIMEKABIDHI MSAADA WA SARUJI

 

Shirika lisilokuwa la kiserikali green light foundation  limekabidhi msaada wa mifuko mia moja(100) ya saruji yenye thamani ya shuilingi milioni moja laki tano (1,500,000) kwa ajili ya ujenzi wa skuli ya ghorofa ya Mtambile katika Wilaya ya Mkoani Pemba.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Muheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla Mkurugenzi wa NGOs hio Salim Mussa Omar amesema shirika hilo limefanya hivyo ili kutoa mchango wake kwa maendeleo ya Taifa.

Amesema Taifa lolote hujengwa na wananchi wenyewe na hasa katika kusaidia Vijana kupata elimu, hivyo ametowa wito kwa watu wengine wenye uwezo popote walipo kufanya hivyo  ili kujenga Taifa bora.

Amesema shirika hilo linajishughulisha na utoaji wa huduma za afya na elimu hasa Vijana kujiendeleza kimaisha.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Muheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla amempongeza  Mkurugenzi wa Green light Foundation kwa msaada huo na mengine aliyowahi kuitoa na kusema kuwa itasaidia juhudi a wananchi wa mtambile kuendeleza ujenzi wa skuli yao.

Nae Katibu wa Kamati ya Ujenzi wa Skuli ya Mtambile ndugu Hassan Bakar amemshukuru Mkurugenzi huyo kwa msaada alioutoa na kuahidi kuwa utatumika kama ulivyokusudiwa.