SHUGHULI ZA UJENZI KATIKA ENEO LA SKULI YA BUMBWINI KUSITISHWA

 

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘B’ ndugu Rajab Ali Rajab amesitisha shughuli za ujenzi katika eneo la skuli ya bumbwini makoba na kuitaka jamii kuheshimu maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za kijamii ili kuepusha migogoro.

akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea shehiya  zenye migogoro ya ardhi  kiomba mvua na makoba amesema serikali ya wilaya haipo tayari kuona migogoro ya ardhi inajitokeza katika jamii kwa kuwepo baadhi ya watu kushindwa kuafata taratibu za umiliki wa ardhi.

amefahamisha kuwa katika kutatua matatizo hayo atashirikiana na idara ya ardhi ili kubainisha mipaka sahihi ya kila  eneo   pamoja na  hati miliki ya maeneo  hayo.

kwa upande wake sheha wa shehiya ya kiomba mvua ndugu muhammed ali ame amewataka wananchi kushirikisha pande zote kabla ya kuanza kwa shughuli za ujenzi katika maeneo yao ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.