SITISKANI ILIYOHARIBIKA MAPEMA MWEZI HUU ITAFANYIWA MATENGENEZO

 

 

Serekali ya  mapinduzi ya zanzibar imesema  mashine ya kuchunguzi a wagonjwa kwa picha sitiskani  iliyoharibika  mapema mwezi huu itafanyiwa matengenezo haraka iwezekanavyo ili kuwaondoshea usumbufu wananchi wanaohitaji huduma hiyo.

Akizungumza  na  waaandishi wa habari kaimu mkuurugenzi mkuu wa hospitali   ya mnazi  mmoja dr msafiri  marijani amesema  mashine hiyo  serekali tayari imeshaagiza kifaa hicho kilicho haribika kinachojulikana kwa jina la a exray  tub  ambacho kimegharimu zaid ya dola za kimarekani  elfu 65.

amesema kwa sasa wajonjwa watakao hitajika kutumia kipimo hicho wanatumia  kipimo cha dharura ( mri )  hasa kwa  waokuwa wagonjwa mahatuti  kama waliopata  ajali na kuongeza kuwa  mashine za exray na utrasaund zina fanya kazi kama kawaida .

Hata hivyo dr msafiri  amewasihi wananchi kuwa na subra wakati  serekali inaendelea na  jitihada za  kulimaliza tatizo hilo.