SKULI YA LUMUMBA KUWEKA MIKAKATI YA KUHAKIKISHA INAINGIA NAFASI YA KUMI BORA TANZANIA

 

 

Skuli ya sekondari ya lumumba  imesema imeanza kuweka  mikakati kabambe  ya maandalizi   kuhakikisha inaingia   nafasi ya   kumi bora tanzania  kufuatia kufanya vizuri    mitihani iliyofanyika mwishoni mwa  mwaka jana.

Imesema uamuzi huo umeweza kuyafikia malengo  ya serikali na wazee katika kuviendeleza vipaji vya  masomo kwa wanafunzi.Mwalimu mkuu wa skuli hiyo mussa hassan mussa ameiambia zbc kwamba   kwa kuwa matokeo hayo yameonyesha kuwa vinara kwa kuongoza lumumba  kwa skuli za  zanzibar  bila ya kupata  mpinzani hivyo wameamua kutoa ushindani kwa  tanzania bara katika kufanya vyema kuanzia mwaka huu.

amesema skuli ya lumumba  imejipanga   kwa  kuwa na  vifaa vya kutosha vya maabara     ikiwemo  walimu na vitabu na kwamba  hakuna  sababu yakutokuwa  na ushindani  wa masomo katika sekta ya elimu nchini. kufuatia  kufanya vyema mwalimu wa skuli hiyo  bi fatma aliy mmanga ameishauri wizara ya elimu na mafunzo ya amali  kuzidi kuwachagua wanafunzi   wa vipawa  pamoja na masomo ya sayansi huku akiitaka wizara hiyo kuwa na utaratibu wa kuitembelea kujua changamoto zinazoikabili skuli hiyo.

Wanafunzi wa  kidato cha tano wa skuli hiyo wamesema matokeo hayo yametokana na juhudi zao   za kusoma   pamoja na ushirikiano  huku wakiishauri wizara ya elimu kufanya utafiti juu ya skuli nyengine ambazo hazikupata ufaulu mzuri  baada ya kufanya mitihani yao.Skuli ya lumumba imekuwa ya kwanza   kwa zanzibar   kutoa wanafunzi wa  kidato cha nne  ambapo  skuli ya fidel castro pemba inashika nafasi ya kwanza  kwa wanafunzi wa kidato cha pili  huku lumumba ikishika nafasi ya pili.