SMZ HAITAMVUMILIA MTU YEYOTE ATAKAE HUJUMU UCHUMI

 

 

serikali ya mapinduzi ya zanzibar imesema haitamvumilia mtu yeyote atakae hujumu uchumi wa nchi.

waziri wa fedha na mipango dk khalid salum mohamed amesema hayo katika semina ya siku moja kwa masheha na madiwani juu ya uhamasishaji wa mkuza  awamu ya tatu iliyofanyika katika ukumbi wa makonyo wavi pemba.

amesema kuna baadhi ya watendaji  waliopewa dhamana baadhi ya wakati wanasahau wajibu wao.

waziri huyo amewataka viongozi hao kutoa elimu kwa  wananchi juu ya ukusanyaji wa mapato.

hata hivyo dk halid amesema serikali itahakikisha inaongeza usimamizi katika masuala yote ya smz.

mkuu wa mkoa wa kusini pemba mh hemed suleiman amesema viongozi na wananchi wa mkoa wake watahakikisha wanashirikiana

katika uwelewa na kuwa na ari nguvu na kasi kubwa ya kuleta maendeleo katika nchi.

wakitoa michango yao washiriki wa semina hiyo wametoa shukrani kwa serikali kupitia wizara ya fedha kwa elimu wioipata juu ya mkuza awamu ya tatu.

mada tano ziliwasilishwa na wakufunzi k utoka  taasisi mbali mbali za serikali ambapo semina hiyo imetewa kwa mikoa yote ya unguja na pemba juu ya uhamasishaji wa mkakati wa kupunguza umaskini zanzibar mkuza awamu ya tatu.