SMZ IMESEMA HAITARUDI NYUMA KATIKA KUIMARISHA USTAWI WA WAZEE HAPA NCHINI

 

 

Serikali   ya  mapinduzi  ya  zanzibar imesema  haitarudi  nyuma katika kuimarisha  ustawi  wa  wazee hapa nchini kwani  ni jukumu muhimu kwa serikali inayojali watu  wake.

Waziri  wa  kazi , uwezeshaji , wazee , wanawake  na  watoto  mh. Moudeline castico  ametoa  tamko  hilo  wakati akizindua  baraza   la  kwanza  la  wazee  katika jimbo  la  magomeni lenye  dhamira  ya  kusimamia  maslahi  yao.

Waziri  castico  amesema  wazee  bado   ni  hazina na  tunu  ya  taifa   na kusisitiza   kuwa  serikali  iatazidisha juhudi kuhakikisha wazee wanaishi  maisha bora  na  kupata stahiki  zao.

Ametoa rai   kwa  wadau  mbali mbali katika  jimbo  la  magomeni  kulitumia  baraza   la   wazee  kupambana  na   ongezeko  la  vitendo  vya  udhalilishaji  kwa wanawake  na  watoto.

Wakizungumza katika uzinduzi  huo mwakilishi   wa jimbo la magomeni mh. Rashid makame shamsi   na  mbunge   jamal kassim  ali  wamewahakikishia  wazee kuwa watafanya kila  juhudi kumaliza changamoto  zinazowakabili  na  upatikanaji  wa  stahiki zao.

Katika   risala  yao  wazee  wamesema  lengo  la   baraza  hilo   ni kuwaunganisha  wazee  wapatao 850 jimboni   humo  ili kuimarisha  maisha  yao.