SMZ INAWATHAMINI VIJANA WANOTAKA KUITUMIKIA NCHI NA TAIFA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  ambaye pia ni mwakilishi wa Jimbo la Chwaka Issa Haji Ussi amesema  bado serikali ya mapinduzi ya zbar inawathamini vijana uwepo wao wanaoutoa katika kuitumikia nchi na taifa kwa ujumla   na ndipo serikali  ikaanzisha mabaraza hayo ya  vijana kwa kutambua mchango wao   ili kuona wanashirikishwa katika ngazi mbali   katika kutoa maamuzi yaliyo  sahihi ambayo yataweza kufanyiwa kazi na kuleta maendeleo.  Na kuwataka vijana hao kuondosha wasiwasi ya kuwa kero nyingi hazisikilizi na kupatiwa ufumbuzi .\

Akifungua Mdahalo juu ya ushirikishwaji wa vijana katika siasa na ngazi za maamuzi  kwa vijana wa wilaya ya mjini na kati pamoja na masheha na wawakilishi. Ulioandaliwa na jumuia ya wanasheria wanawake zafela .

Amesema mara nyingi  vijana ndio nguzo ya Taifa hivyo ni vizuri kuwashirikisha katika kutoa maamuzi kwenye siasa  yaliyo mazuri  ambayo yatapelekea kulinda amani ya nchi na kujiepusha na uchochezi. Na kujiepusha na makundi yanayoaashiria uchochezi

Huku akiwataka vijana kuitumia fursa  ziliopo kwa umakini zaidi na kutoa michango yao pamoja na changamoto zinazowakabili kuzieleza ili ziweze kufanyia ufumbuzi kwa ufanisi na kuweza kupatikana  kwa Maendeleo

 

Nae Mwenyekiti  wa Chama cha Wanasheria wanawake zafela  Safia Hijja Abas alisema chama chao kiko mbele katika kuwalinda wanawake na watoto katika masuala ya udhalilishaji na kuhakikisha wanashirikiana na Serikali katika kutolewa maamuzi yanayostahiki kwenye udhalilishaji huo. Paused

Nao vijana hao wakaelezea kero zao mbali mbali ambazo zimekuwazikiwakabili na bado hazijatafutiwa ufumbuzi wa kina  na kupelekea kukosa mustakibali mzuri wa maisha yao. Paused kwa upande wa wakilishi walioshiriki katika mdahalo huo  akiwemo mhe said dimwa amesema ipo haja ya kubadilishwa kwa sheria ya vijana kwani imeonekana kuwa na mapungufu na mhe ahmada   ameseama kero za vijana wamezipokea na kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi wake .

 

Mdahalo huo wa siku moja  umeandaliwa na Chama cha wanasheria  wanawake ZAFELA  kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la foundation for civil society.