SMZ ITAENDELEA KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imesema itaendelea kuimarisha sekta ya elimu ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata haki hiyo katika mazingira bora.
Waziri wa elimu na mafunzo ya amali mh. Riziki pembe juma akikabidhi sare za skuli kwa wanafunzi wa skuli ya mgonjoni ikiwa ni hadi ya rais wa zanzibar, amesema wizara itaendelea kuwa karibu na kijiji hicho ili kupata mafanikio ya haraka kielimu.
Mh riziki amewasisitiza wazazi kuwashajihisha watoto kupenda masomo ili lengo la serikali la kuhakikisha watu wanaondokana na ujinga linafanikiwa.
Afisa elimu maandalizi na vituo vya tutu bi fatma mode ramadhan amewataka wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao na kuhakikisha hawajishirikishi na vitendo viouvu.
Sheha wa shehia ya kilombero mohd haji faki ameshukuru msaada huo ulioahidiwa na dk. Ali mohd shein wakati akiweka jiwe la msingi wa skuli hiyo kuwa una mchango mkubwa kwa sekta ya elimu.