SMZ ITAENDELEA KUONGEZA HUDUMA ZA KIJAMII KWA WAZEE WALIOTOA MCHANGO KWA YA TAIFA.

Waziri wa Ardhi maji Nshati na mazingira Mh. Salama Aboud Talib, amesema serikali itaendelea kuongeza huduma za kijamii kwa wazee waliotoa mchango   kwa maendeleo ya taifa.

akifungua kikao cha halmashauri kuu ya umoja wa maaskari wastaafu huko kijangwani, amesema miongoni mwa huduma hizo ni kuwaweka karibu ilikuweza kupata michango katika kuendeleza nchi.

Mh. Salama ameuomba umoja huo wa wastaafu kushirikiana kwa pamoja katika kuweka mikakati ya kuwaeleimisha vijana juu ya umoja na mshikamano pamoja na kulinda amani ya nchi.

mwenyekiti wa umoja wa maaskari wastaafu  kanal Miraji Mussa Vuai  amesema jumuiya hiyo imewasidia kubuni miradi ya kujiendeleza kiuchumi inayowawasaidia katika maisha yao.