SMZ KUAJIRI WATUMISHI MIA NNE HAMSINI NA TANO

 

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imesema inatarajia kuajiri watuishi mia nne hamsini na tano baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo jipya la abiria katika kiwanja cha abeid aman karume (treminal  iii).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara ya kutembelea ujenzi huo  waziri wa ujenzi mawasiliano na usafirishaji dr,sira ubwa mamboya amesema vijana wajiweke tayari kwa ajira hizo..

Amesema serikali imekusudia kuwapa elimu vijana watakaobahatika kupata ajira hiyo ili waweze kuendana na mahitaji ya huduma zitakazo tolewa katika kiwanja hichi cha kimataifa.

Dk.sira amesema jenzi huo unaendelea vizuri na serikali imeridhika na hatua iliyofikia ambao utaimarisha zaidi huduma za ndege kubwa zinazobeba watalii wanaoingia nchini kila mwaka.

Kwa upande wake  mratibu wa serikali  wa jengo hilo bw, yasser de costa amesema watahakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilika kwa wakati.