SMZ KUFIKIA KATIKA KIPATO CHA KATI IFIKAPO 2020.

 

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais mh.muhammed aboud amesema dhamira ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar ni kufikia katika kipato cha kati ifikapo 2020.

Waziri aboud amesema matumaini makubwa yapo katika kufikia lengo hilo kutokana na wananchi wengi kupata maendeleo baada ya kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo ya jamii tasaf uliowezesha kujikwamua kimaisha.

Mh. Aboud ameyaeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kikao cha ripoti ya utekelezaji wa miradi ya tassaf kwa ujumbe wa benki ya dunia.

Mjumbe wa benki ya dunia anaesimamia miradi ya tasaf tanzania.mohamed modeliste amesema lengo la kuja tanzania ni kufanya tathmini ambayo itasaidia kufikia maamuzi ya kuidhinisha mpango wa mradi huo awamu ya tatu katika hatua ya pili na ameelezea kuridhishwa na utekelezaji wa mpango huo wa tasaf kwa tanzania.

Wakati huo huo ujumbe huo umefika katika kijiji cha bumbwini shehia ya mafufuni kukagua mradi wa bwawa la samaki na kupata maelekezo kwa mtaalam anaesimamia bwawa hilo.