SMZ KUMALIZA MRADI WA UJENZI WA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA

 

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imeshauriwa kumaliza mradi wa ujenzi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa abeid aman karume terminal 2 ili kufikia lengo la utoaji wa huduma bora katika uwanja huo.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege tanzania salim msangi, ametoa ushauri huo mbele ya kamati ya ardhi na mawasiliano ilipotembelea mradi wa ujenzi wa upanuziterminal 3 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere jijini dar es salam.

Amesema uwepo wa kiwanja cha ndege chenye hadhi utaongeza pato la zanzibar kwa kuongeza idadi ya ndege zitakazotua kwenye kiwanja hicho na idadi ya abiria hususan watalii.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hamza hassan juma amepongeza hatua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa terminal 3 ambao umefanyika kwa fedha za ndani na kusifu kitendo cha ushirikishwaji wadau katika utekelezaji wa mradi huo.

Kamati ya ardhi na mawasiliano ya baraza la wawakilishi pia imetembelea mamlaka ya usafiri wa anga tanzania (taa) na mamlaka ya hali ya hewa tanzania (tma) ikiwa ni muendelezo wa ziara yake jijini dar es salaam.