SMZ KUTEKELEZA SERA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASIKINI

 

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania mh. Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar inajitahidi kutekeleza sera mbali mbali ili kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa wananchi wake.

Akifungua soko la konde lililojengwa kupitia program ya miundombinu ya masoko mheshimiwa samia amesema suala la kupunguza umasikini ni ajenda kuu ya taifa hivyo ni jukumu la serikali kuweka mazingira bora kwa wananchi ili waweze kujiletea maendeleo yao.

Nae katibu mkuu wizara ya kilimo ndugu joseph abdalla meza amesema utekelezaji wa mradi huu ni muendelezo wa mashirikiano baina ya smz na smt na hii ni kudhihirisha kwamba serikali mbili hizi zinafanya kazi kwa pamoja kwa  maslahi ya wananchi wake na kwa upande wa gharama za ujenzi wa soko hilo amesema.

Nae waziri wa kilimo mali asili mifugo na uvuvi mh. Hamad rashid mohammed amempongeza rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi kwa jitihada zake za kupeleka maendeleo sawa kila pahala katika visiwa hivi.

.