SMZ KUTUMIA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI THAMANINI NA TATU KUWALIPA FIDIA WANANCHI WALIOANGUKA WAKATI WAKICHUMA KARAFUU

Serikali ya mapinduzi zanzibar imesema imetumia zaidi ya shilingi milioni thamanini na tatu kuwalipa fidia wananchi walioanguka wakati wakichuma zao la karafuu katika kipindi cha mwaka 2015/2016.
Akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la chake chake mhe, suleiman sarahani said katika kikao cha baraza la wawakilishi, waziri wa biashara viwanda na masoko mhe, amina salum ali amesema wengi wa walioanguka wakichuma karafuu ni kutoka mkoa kaskazini pemba na kwamba kwa mujibu wa sheria ni lazima walipwe fidia.
Amesema kwa mwaka huu serikali imetenga shilingi milioni 127 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi watakaopata ajaili za kuanguka wakiokoa zao hilo la uchimi kwa zanzibar.
Amefahamisha kwamba serikali imepanga utaratibu mzuri wa kuwalipa fidia watakaoanguka wakichuma karafuu lakini amesisitiza wananchi kuwa na tahadhari wakati wakifanya kazi hiyo.
Kuhusu magendo ya karafuu waziri amina amesema serikali imejipanga vyema kiulinzi hasa kisiwani pemba ili kuhakikisha hazitoroshi na wafanyabiashara wakorofi wasiojali uzalendo.
Wakati huo huo naibu waziri wa kilimo maliasili mifugo na uvuvi mhe, lulu msham khamis amesema wizara yake inafanya juhudi ya kupanda mikarafuu mipya katika mashamba kadhaa ya mikarafuu huko konde ili kujaza nafasi ya iliyokufa kutokana na umri mrefu.
Katika hatua nyingine waziri wa nchi afisi ya makamo wa pili wa rais mhe, mohammed aboub amesema asilimia thamanini ya wananchi wa zanzibar wanapata maji safi na salama katika nyumba zao kutokana na juhudi kubwa inayofanywa na serikali.
Hata hivyo amewata viongozi kuendelea kuwasaidia wananchi kwa kuwatatulia matatizo yao mbali mbali yanayowakabili ili wafaidike na matunda ya utekelezaji wa ilani ya ccm sera na serikali ya mapinduzi.