SMZ KUZIFANYIA MAPITIO SHERIA ZINAZOSIMAMIA ZAO LA KARAFUU

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshauriwa kuzifanyia mapitio sheria mbali mbali zinazosimamia zao la karafuu zanzibar kwa lengo la kudhibiti magendo ya karafuu na kuwapunguzia wakulima changamoto zinazotokana na mapungufu ya sheria hizo

ushauri huu umetolewa na katibu wa jumuiya ya wazalishaji karafuu zanzibar (zacpo) ndugu abubakar mohd ali katika warsha ya uwasilishaji wa matokeo ya utafiti wa mapitio ya sheria mbali mbali zinazosimamia zao la karafuu zanzibar ulifanyika katika ukumbi wa uwanja wa makonyo chake chake pemba.

akiwasilisha matokeo ya utafiti huo, mtafiti, dk deogratius mahangila kutoka chuo kikuu cha dar es salaam, katika kitengo cha biashara amesema kuwa utafiti umebaini karafuu nyingi zinapotea kisiwani pemba kutokana na zuio la wananchi kuchuma na kuanikia karafuu zao sehemu tafauti

wakichangia katika warsha hiyo wakulima wa karafuu na wananchama wa jumuiya hiyo wamesema kuwa uwelewa wa sheria hizo kwa baadhi ya wasimamizi ni mdogo jambo ambalo hupelekea  kutokea changamoto nyingi kwa wakulima

katika warsha hiyo ambayo imewashirikisha wakulima wa zao la karafuu, maafisa wa taasisi mbali mbali na wananchama wa jumuiya ya uzalishaji wa karafuu zanzibar kutoka unguja na pemba, mapendekezo mbali mbali juu ya kuzifanyia marekebisho sheria hizo yaliwasilishwa na kukubali